BAADA ya habari kuzagaa kwenye mitandao ya kijamii na mwanamuziki Naftal Mlawa ‘Nuh Mziwanda’ kuandika katika ukurasa wake kwamba alilala na mpenzi wake wa zamani, Zuwena Mohamed ‘Shilole’ wiki moja kabla ya kufunga ndoa, mwanamama huyo ameibuka na kumtolea maneno makali.
Akipiga stori na Mikito Nusunusu, Shilole ambaye alifunga ndoa na Uchebe wiki iliyopita alisema, Nuh ni sawa na mfa maji asiyeisha kutapatapa hivyo anatakiwa kupambana na hali yake.
“Sitaki kumzungumzia Nuh kwa sababu mimi na mume wangu tunamuona ni mfa maji anayetapatapa tu, namshauri tu apambane na hali yake aache kufuatilia na kutaka kuharibu maisha ya watu,” alisema Shilole.