Harmorapa Afunguka Ukaribu Wake na Meneja Wake - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Dec 2017

Harmorapa Afunguka Ukaribu Wake na Meneja Wake

Harmorapa Afunguka Ukaribu Wake na Meneja Wake
Akiongea na mtangazaji wa kituo cha redio cha Sunrise 94.9 FM kilichopo mkowani Arusha maarufu kama Lee Baibe, Harmorapa aliweka wazi kwenye dawati la kipindi cha burudani cha Flava Plus kinachoondeshwa na watangazaji DJ. Dix na Lee baibe kuwa uhusiano wake na maneja wake Bi Irene Sabuka kuwa upo imara. Kumekuwa na tetesi yakuwa rapper huyu ambae aliparamia umaarufu kwa ghafla na amekua mmoja wa mastaa ambao kwa lugha ya kisasa inasemekana wanatamba kwa kiki. Harmorapa amepinga tetesi zakua anapitia kipindi kigumu kisa na maana wamekosana na maneja wake Irine Sabuka. Hali iliyopelekea Lee Baibe kumutafuta kupitia njia ya simu na moja kwa moja kumuhoji hewani.

Awali Harmorapa alikuwa ametupia maneno yenye kuleta mshikli kupitia akaunti yake ya instagram yenye zaidi ya wafuasi lakimoja, ambapo wengi wa mashabiki wake waliyatafrisi kuwa huenda uhusiano wake na usimamizi wake ukawa upo kwenye njia panda. Nikinukuu waraka huo ‘‘harmorapatz1Kila Jambo lina Muda wake maalumu kamwe lipangwalo Na Mungu hakuna Binadamu wakuzuia ..Naamini na Hili limepangwa na Muda likapewaWacha lichukue Nafasi yake sasa.. Muda ukifika nitapewa nilicho andaliwa#Newharmorapaintown”  Staa huyo pia amewataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kwani huenda wakati wowote akaliamusha dude.