Rekodi ya Arsenal Yavunjwa na Manchester City - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Dec 2017

Rekodi ya Arsenal Yavunjwa na Manchester City

Rekodi ya Arsenal Yavunjwa na Manchester City

USHINDI wa mabao 4-0, dhidi ya Swansea City umeifanya Manchester City kuvunja rekodi ya Arsenal ya kushinda mechi nyingi mfululizo katika Premier League.


Man City sasa imeshinda mechi 15 mfululizo na kuivuka Arsenal ambayo ilikuwa ikishikilia rekodi ya kushinda mechi 14 mfululizo lakini yenyewe ilifanya hivyo katika misimu miwili tofauti wakati City wao wamefanikisha ndani ya msimu mmoja.

Pamoja na rekodi hiyo bado City ina nafasi ya kuweka rekodi zaidi ya hapo kwa kuwa inaendelea kucheza.
Kwa takwimu hizo pia Man City imekuwa timu ya nne kwa Ulaya kushinda mechi nyingi mfululizo katika ligi kuu.