Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na baadhi ya viongozi wamefika nyumbani kwa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam kumfariji baada ya kufiwa na mke wake Peras Ngombale hivi karibuni na anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kinondoni.
Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya jana. Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam jana.
Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale Victoria, jijini Dar.
11 Jan 2018
New
mulo
Kingunge