Refa Amrushia Teke Mchezaji Kisha Kumpa Kadi Nyekundu - MULO ENTERTAINER

Latest

16 Jan 2018

Refa Amrushia Teke Mchezaji Kisha Kumpa Kadi Nyekundu


SeeBait
Refa Amrushia Teke Mchezaji Kisha Kumpa Kadi Nyekundu

Mwamuzi huyo Tony Chapron alifanya hivyo baada yake kugongana na mchezaji huyo Diego Carlos.


Baada ya hilo, alimlisha mchezaji hiyo kadi ya pili ya manjano na kumfukuza uwanjani kufuatia kisa hicho muda wa ziada wa mechi.

Mwenyekiti wa Nantes Waldemar Kita amesema Chapron anafaa kupigwa marufuku kwa miezi sita kwa sababu ya uamuzi huo wenye utata.

PSG walipokuwa wanashambulia eneo la hatari la Nantes, Carlos alimgonga Chapron kwenye kisigino katika kile kinachoonekana kuwa ajali.

"Ni mzaha," Kita aliambia runinga moja ya Ufaransa.

"Nimepokea arafa 20 kutoka pande mbalimbali duniani kuniambia kwamba huyu mwamuzi ni mzaha tu.

"Nikizungumzia hili sana, nitaitwa kujibu maswali na kamati ya maadili. Hatuna haki ya kusema chochote."

PSG walishinda mechi hiyo yao ya kwanza baada ya mapumziko ya msimu wa baridi, bao lao pekee likifungwa na Angel di Maria dakika ya 12 uwanjani Stade de la Beaujoire.

Ushindi huo, bila mchezaji wao ghali zaidi Neymar aliyenunuliwa £200m - uliwaweka alama 11 mbele kileleni Ligue 1.

Meneja wa Nantes Claudio Ranieri alisema: "Jambo mbaya zaidi litakalomtendekea Diego Carlos ni kwamba atapigwa marufuku kucheza mechi moja. Ilikuwa mechi nzuri kwetu tukisahau bao ambalo lilikataliwa kwa sababu ya kuotea na pia yaliyomsibu Diego Carlos."