Msanii wa muziki wa Injili Bongo, Emmanuel Mbasha amejibu kuhusu tuhuma za kuazima magari ya watu kwa ajili kupiga picha ili kujionyesha katika mitandao.
Muimbaji huyo amesema tuhuma hizo hazina ukweli wowote kwani kazi zake anazozifanya zinatosha kumuingiza kipato cha kuweza kumiliki magari kadhaa.
“Hamna, mimi huwa siazimi magari, yote niliyona ni ya kwangu, ninatumia gari zangu na watu wa karibu yangu wanafahamu mimi ni mfanyabiashara, ninaimba Gospel na nina kipato cha kufanya mambo yangu yote ya unayoyaona,” Mbasha ameiambia Bongo5.
Ameongeza kuwa kwa sasa anamiliki magari mawili. Wimbo wa mwisho Mbasha kutoa ni Hallelujah ambao amemshirikisha Hondwa, wimbo huo ulitoka October 2017.
26 May 2018
New
Akanusha Tuhuma za Kuazima Magari: Emmanuel Mbasha
mulo
Newer Article
BREAKING: Mbunge Kasuku Wa Buyungu Kigoma Kupitia CHADEMA Afariki Dunia
Older Article
Dunia Kusimama kwa Dakika 90 Kuiona Real Madrid vs Liverpool hii leo
Labels:
Bongo Land,
Udakuzi