Leo May 26, 2018 Taarifa iliyotufikia hivi punde ni kuwa Mbunge wa jimbo la Buyungu mkoani Kigoma, Kasuku Samson Bilago (CHADEMA) amefariki dunia mchana huu katika Hospitali ya Taifa, Muhimbili.
Kupitia ukurasa wa Twitter wa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amethibitisha
Marehemu Bilango alikua anakabiliwa na maradhi ya utumbo, ambapo alisafirishwa kwa ndege maalum kutoka Dodoma kuja Dar es Salaam siku ya jumanne.
Mwalimu Bilago amekuwa akisumbuliwa na ugonjwa huo kwa wiki nzima sasa ambapo awali alilazwa katika hospitali moja ya Kanisa mjini Dodoma.
Marehemu alizaliwa February, 2 mwaka 1964 na alichaguliwa kuongoza jimbo hilo mwaka 2015.