BREAKING: Watu 19 Wamefariki Katika Ajali ya Basi na Lori - MULO ENTERTAINER

Latest

26 May 2018

BREAKING: Watu 19 Wamefariki Katika Ajali ya Basi na Lori

Watu wasiopungua 19 wamefariki na wengine kadhaa kujeruhiwa May 26, 2018 wakati basi walilokuwa wakisafiria kugongana na lori katika wilaya ya Kiryandongo magharibi mwa Uganda.

Miongoni mwa waliofariki kulikuwa na watoto watatu na watu wazima 16, taarifa kutoka kwa maafisa wa polisi ilisema.

“Timu ya uokoaji wanafanya kazi bila kuchoka ili kuwaokoa majeruhi na kuwapeleka katika hospitali ya Kiryandongo,” taarifa hiyo ambayo iliyotolewa na msemaji wa polisi, Emilian Kayima, ilisema.