Mashindano ya Kufanya Sura Kuwa Mbaya - MULO ENTERTAINER

Latest

26 May 2018

Mashindano ya Kufanya Sura Kuwa Mbaya

Dunia ina vituko sana unaambiwa hivi huko nchini Uingereza kuna mashindano ya kufanya sura kuwa mbaya (Gurning Competitions) sasa leo May 26, 2018 nakusogezea mmoja wa washindi wa kihistoria  wa mashindano hayo anayejulikana kama Anne Woods ambaye ameshinda mashindano hayo mara 27 katikati ya miaka ya 1977 mpaka 2010.



Aidha duru zinasema kuwa familia yake ndio ilimuingiza Anne kwenye mashindano hayo mwaka 1977 na kwa sasa amestaafu kushiriki mashindano hayo.

Mashindano hayo yalianzishwa mwaka 1267 nchini Uingereza na hufanyika kila mwaka mwezi September huko Egremont,Cumbria nchini Uingereza.