Dk Shoo: Kanisa Limekuwa Msaada - MULO ENTERTAINER

Latest

28 May 2018

Dk Shoo: Kanisa Limekuwa Msaada

Dk Shoo: Kanisa Limekuwa Msaada
Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo amesema kanisa limekuwa msaada kwa wananchi na linawasaidia kutatua changamoto zinazowakabili.

Akizungumza jana katika uzinduzi wa Jubilee ya miaka 125 tangu kuingia kwa injili Kanda ya Kaskazini, Askofu Shoo alisema katika kipindi hicho cha miaka 125 kumetokea mabadiliko mengi katika mfumo wa maisha.

“Neno kuu la Jubilee hii, linatoka katika kitabu cha Yeremia 22:29, lakini naomba tutambue kuwa kanisa limekuwa msaada mkubwa kwa wananchi,” alisema Askofu Shoo.

Jubilee hiyo ilifanyika katika Usharika wa Ashira, Dayosisi ya Kaskazini.

Awali, akihubiri katika ibada hiyo, Askofu wa Dayosisi ya Kaskazini Kati, Dk Solomon Massangwa alisema Wakristo wanapaswa kuondokana na matendo yote yasiyofaa na kujitwika utu upya.

Dk Massangwa alisema kuyaacha matendo yasiyofaa, ni kuwa na matumizi mazuri ya rasilimali kwa kizazi cha sasa na kijacho.