Watu 45 wameathirika baada ya kuvuta hewa yenye sumu kutoka kiwanda cha kutengeneza sabuni cha ROYAL kilichopo Mabibo external Jijini Dar es Salaam.
Akitibitisha kutoka kwa tukio hilo, Mkuu wa wilaya ya Ubungo Bw. Kisare Makori amesema tatizo hilo limetokea baada ya kuwepo kwa hitilafu katika moja ya mtambo wa kuchuja tindikali lakini mpaka sasa, wamiliki wa kiwanda hicho wameshadhibiti na zoezi la uzalishaji linaendelea kama kawaida.
"Kuna watu watatu ambao walipata madhara zaidi yaani walikuwa wanatapika na kuumwa vichwa lakini wameshapatiwa matibabu na wengine 42 walienda katika kituo cha afya kupatiwa huduma kutokana na kuhisi kuathirika na hewa hiyo waliyoivuta wakati wakiwa kiwandani", amesema Makori.
23 May 2018
New
Watu 45 wamevuta hewa yenye sumu Dar es salaam
mulo
Newer Article
Neema yawaangukia Barack Obama na mkewe, wasaini dili nono na kampuni ya Netflix
Older Article
Kamanda wa Polisi aliyewaonya wanaume kukohoa azungumzia kuhamishwa kwake ghafla baada ya kauli hiyo
Polisi Tanzania kuajiri askari wapya 3,000Aug 13, 2021
Habari kubwa za Magazeti ya Tanzania May 23 May 23, 2019
Labels:
Habari