TRA Yaweka Wazi Kuhusu Kulipia Kodi Mtandao wa Whatsapp - MULO ENTERTAINER

Latest

3 Jul 2018

TRA Yaweka Wazi Kuhusu Kulipia Kodi Mtandao wa Whatsapp

TRA Yaweka Wazi Kuhusu Kulipia Kodi Mtandao wa Whatsapp
Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), imekanusha taarifa zinasombazwa kupitia mitandao ya kijamii zilizodai kuwa mtandao wa ‘whatsapp’ utaanza kulipiwa kuanzia Julai 10, mwaka huu.

Kupitia taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, Mamlaka ya Mapato (TRA), Richard Kayombo imesema kuwa taarifa hizo zinazodai kuwa mtandao huo utaanza kulipiwa kiasi cha shilingi elfu 15 kuanzia Julai 10 hazina ukweli wowote.

“Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA), inapenda kuufahamisha Umma kuwa, taarifa zinazosambazwa katika mitandao ya kijamii zikidai kwamba Mtanzania yeyote anayetumia whatsapp atatakiwa kulipia shilingi 15,000/= kuanzia tarehe 10 mwezi huu ni za uongo”, imesema taarifa.

Mamlaka hiyo imetoa wito kwa watumiaji wa mtandao ya kijamii kuwa makini na kupuuza taarifa hizo kwakuwa hazina ukweli wowote.