Kikosi cha Azam FC kinashuka Uwanjani leo 'Mwadui Complex' kuanza safari yake ya kupigania alama 9 kanda ya ziwa kwa kucheza na Mwadui FC.
Kuelekea mechi hiyo, Azam itamkosa kiungo wake Tafadzwa Kutinyu ambaye alichelewa kuripoti kambini kutokana na majukumu ya timu ya taifa.
Kutinyu alisafiri kuelekea Zimbambwe kuitumikia timu yake ya taifa kwa ajili ya kuwania kusaka tiketi ya kufuzu kuelekea AFCON na kusababisha achelewe kurejea kwa ajili ya kujiandaa na kambi kuelekea mechi hiyo.
kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam, Jaffer Idd Maganga, amesema Kutinyu hataweza kuwepo kwenye kikosi kitakachoshuka kumenyana na Mwadui leo.
Baada ya kumalizana na Mwadui, Azam itakuwa ina vibarua vingine viwili dhidi ya Stand United na Biashara United kisha Alliance ya Mwanza.