Esma Atoa ya Moyoni Kuhusu Petit Man "Niliachana Naye Kabla ya Ishu za Kuchepuka na Mnyarwanda'' - MULO ENTERTAINER

Latest

13 Sept 2018

Esma Atoa ya Moyoni Kuhusu Petit Man "Niliachana Naye Kabla ya Ishu za Kuchepuka na Mnyarwanda''

Esma Athibitisha Kuachana na Petit Man "Niliachana Naye Kabla ya Ishu za Kuchepuka na Mnyarwanda''
Mdogo wake na Diamond Platnumz, Esma Platnumz amefunguka kwa kudai kwamba ameachana na aliyekuwa mume wake wa ndoa, Petit ambaye alifanikiwa kuzaa naye mtoto mmoja.


Mapema wiki hii Petit Man ambaye alizaa mtoto mmoja na Esma, aliingia kwenye kashfa nzito baada ya kusambaa mtandaoni audio ambayo anasikika akizungumza kimahaba na mwanamke anayedaiwa kuwa wakinyarwanda.

Baada ya sakata hilo, Esma amefanya interview na Wasafi TV na kueleza mengi kuhusu mahusiano yake na Petit Man.

“Kingine ambacho hawakijui mimi na Petit tuliachana muda mrefu hata zile voice note nilivyokuja kuzisikia nilicheka sana halafu akinipigia simu,” alisema Esma Platnumz.

Jumatano hii Petit alifunguka kuzungumzia sakata hiyo na kuonyesha kwamba analifahamu.