Mama Avua Nguo Kumlaani "Serengeti Boy" Aliyegoma Kumlipa Baada Ya Kumpa Penzi - MULO ENTERTAINER

Latest

14 Sept 2018

Mama Avua Nguo Kumlaani "Serengeti Boy" Aliyegoma Kumlipa Baada Ya Kumpa Penzi

Mama mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja amefanya aibu ya mwaka baada ya kusaula (kuvua) nguo zake na kubaki mtupu, kisa kikidaiwa ni kumlaani ‘serengeti boy’ wake aliyemfanyia kitu mbaya.


Kwa mujibu wa chanzo chetu, mwanamke huyo mbali ya kuwa na mtu wake amedaiwa kuwa na tabia ya kuchepuka na wanaume tofauti ambapo amekuwa akifanya hivyo kwa kupanga chumba katika moja ya gesti  iliyopo Sinza kwa Remmy, jijini Dar.

Inadaiwa kuwa tukio hilo lililotokea hivi karibuni, mwanamke huyo kama kawaida yake alipata mteja ambaye ni mdogo kwake kiumri, ambaye pia ni mkazi wa eneo kulikotokea varangati hilo.
“Walikubaliana na huyo kijana kupumzika kwa muda na yule mwanamke katika chumba alichopanga, baada ya kumaliza mambo yao kijana aligoma kumpa hela ndipo mtiti ulipoanzia,” kilisema  chanzo hicho na  kuongeza;

 ”Tulishangaa kuona watu wakivutana huku mwanamke akiwa na kanga moja, ndipo kijana akapata upenyo na kuchoropoka na mwanamke yule akaanza kuvua nguo huku akisema anamlaani kutokana na umri wake kuwa mdogo na kumdhulumu chake.
“Watu walimsihi lakini akawa hasikii zaidi ya kuendelea kuvua na kuamua kumfuata yule kijana kwao huku akiendelea kuvua njia nzima, alipofika kwa yule kijana alianza kugonga geti kwa fujo huku akitoa maneno ikiwemo ya kumlaani.

“Pamoja na makelele na kusaula kote nguo zake lakini hakuambulia kitu zaidi ya kuonesha sehemu zake za siri na baadaye aliamua kuondoka."