Sijawahi kuwa mzinzi tangu nimeoa miaka 5 iliyopita. Hadi hivi karibuni nilipoanzisha uhusiano na binti mmoja..
Tulifahamiana kikazi, yeye yupo idara ya uhasibu. Huja kazini kwangu kila mwisho wa mwezi kwa ajili ya transaction mbalimbali.
Tukazoeana na kuwa wapenzi. Kiukweli mambo yalienda haraka haraka sana na aliingia mazima mazima kiasi kwamba hata kila nilipotaka kumwambia ukweli najikuta nashindwa maana alikua resi ile mbaya.
Ikawa ni mahaba niue, kila tukitoka kazini tupo wote sehemu, weekend tutaenda cinema, beach etc. Yaani ghafla bin vuu anaongelea ndoa. Kila siku ya Mungu lazima agusie ndoa itakua vipi.
Wakati mwingine anaingia Google kusearch magauni ya harusi na viatu na maids wake watavaa nini siku hiyo. yaani nabaki mdomo wazi maana moyoni najua nimeshaoa siku nyingi.
Kila akianzisha hizo story za magauni najitutumua sasa nianze kumwelewesha kwamba nimeoa basi hunikata kauli haraka na kuendelea kusema mambo ya ndoa yetu kwamba napendelea ukumbi gani ndo mzuri.
Sasa tuna miezi miwili ameanza kuongelea suala la kupata mtoto ananiuliza kuwa naonaje akibeba mimba kabisa tufunge ndoa wakati ana mimba. Basi humjibu kuwa tusubiri kwanza asibebe kabisa mimba, nikijibu hivyo anakua mkali anauliza "hiyo mimba unaibeba wewe au mimi?" Mimi nabaki kimya.
Kwa kweli namuonea huruma kwa mawazo aliyonayo, mimi niliingia kwenye huu uhusiano kubadilisha mboga tu and I thought it would be a temporary thing. Kiuchumi yupo vizuri balaa simpati hata kwa dawa.
Ukifika alipopanga thamani za vitu alizonazo ndani ni za gharama sana, na nyumba ni ya kisasa, ana miradi mingi mbali na kazi na alinipeleka anapojenga nyuma ni kama imeisha bado ukuta tu wa nje.
Tatizo pekee ninaloliona ni kuwa huyu binti time is ticking very fast against her age, yupo kwenye mid 30s; somewhere between 30-36 years. Hivyo anadhani amechelewa.
Anasema amepoteza muda mwingi kwenye relationship iliyopita iliyochukua 7 years na jamaa akaoa mtu mwingine na kumuacha yeye, hivyo anasema hataki tena long relationship. Ameshaniunganisha na ndugu kibao. Kila wiki natambulishwa kwa ndugu mpya.
Wakuu, naona huruma Kubreak hii news kuwa nilishaoa. Ingawa nampenda moyoni lakini pia nimechoka maisha ya digi digi ninayoishi maana nikiwa home kwangu usiku lazima anipigie simu na anaongea zaidi ya nusu saa na hapo tumetoka kuonana jioni. Basi najifanya naenda dukani kwa mangi kununua kitu na kupiga stori ili wife asishtuke kuwa naenda kuongea na simu.
I think wengi mnajua maisha ya Ku,cheat yalivyo magumu ni utumwa, ni jela ya nje.
Wakuu nianzeje kumwambia ukweli anielewe? Au nitume mtu mwingine ndo amwambie kama anampa umbea vile?
I need to get out of this mess maana wife somehow ameanza kushtukia mwenendo wangu.