Nyumba ya nini? ndoto yangu ilikuwa Gari - Whozu - MULO ENTERTAINER

Latest

25 Jan 2019

Nyumba ya nini? ndoto yangu ilikuwa Gari - Whozu

Nyumba ya nini? ndoto yangu ilikuwa Gari - Whozu
Baada ya hivi karibuni kuweka wazi kuwa amenunua gari, msanii Whozu amesema kwa upande wake gari ni muhimu kuliko nyumba.

Whozu amefunguka hayo alipokuwa akipiga stori na Clouds FM ambapo ameeleza kuwa gari ni bora kuliko nyumba.

"Kipindi cha mvua hapa Dar es Salaam kuna msemo huwa maarufu sana 'Baba Wenye Nyumba Tujuane', huwa unawakera wale wasio na magari yao binafsi," amesema.

Ameendelea kwa kusema, 'Mimi nyumba ya nini? Gari ukiwa nayo kila mtu atakuona na ilikuwa ndoto yangu kuwa na gari sio kuwa na nyumba,'.