Niamini Mimi Marehemu Godzilah Alikuwa Genius - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Feb 2019

Niamini Mimi Marehemu Godzilah Alikuwa Genius

NUARI 26, mwaka huu, Godzilla aliandika ujumbe Twitter ukasambaa kupita kiasi. Kuna watu wakauchukua na kuutumia pasipo kumpa credit Kingzilla kama ndiye mtunzi halali wa maudhui.

Aliandika: "Pale mnapoamua sasa kutulia na kuanza kuyajenga mahusiano yenu. Ghafla Shetani anaiba simenti." Inachekesha, inafikirisha na inafundisha. Bila shaka unaweza kuwa uliuona ujumbe huu. Basi aliyeandika kwa mara ya kwanza ni Zilla.

Yule Nigga alikuwa na akili sana. Waza aliwaza nini. Hata hivyo ni ukweli kwamba mara nyingi watu huchezeana kwenye uhusiano. Pale mtu anapoamua kutulia aijenge ndoa au penzi lake, anakuta ni "too late". Hapo ndipo Zilla alisema, Shetani kaiba simenti.

Shetani ni mzinguaji sana. Anawavuruga wapendanao. Wanashindwa kuheshimu mapenzi yao. Anamfanya mtu asiione thamani ya mwenzake. Huyu anaruka huku, yule anadikra kule. Kipindi chote cha kurukaruka, kwa Shetani ni kicheko tu. Mbavu hana!

Siku wapendanao wanapojiuliza kwa nini wasitulie wayajenge mapenzi yao? Hapo Shetani huona wapendanao wamemshtukia. Sasa ili kuwakomoa huamua kuiba simenti na kutoka nayo nduki.

Zilla alisema simenti, ukweli ni kwamba kwa wengine Shetani huiba simenti, misumari ya kugongea bati, rangi na vifaa vingine. Matokeo yake wapendanao waliochezea mapenzi yao wanapotaka kuukarabati uhusiano, wanakuta tayari nyufa kibao, aliye nje anaona ndani.

Kwa vile misumari ya kugongea bati nayo imeibwa, basi paa inakuwa inavuja. Mvua ikinyesha wapendanao wanaloa chapachapa. Uhusiano unakuwa hauwasitiri tena wahusika. Jitihada zinakuwa nyingi kuuokoa uhusiano bila mafanikio. Kumbe Shetani ameshaiba zana muhimu za kukarabati uhusiano.

Katika wimbo "Sikati Tamaa Remix" wa Darassa ft Zilla, Joh Makini na Ben Pol. Verse ya kwanza, kuna line Zilla anabomoka: "Machizi hawaamini kama Zilla ni genius." Hapa Zilla alijishtukia tu. Sisi machizi wake tulikuwa tunaamini sana kuwa yeye ni genius. Na hii ni sehemu ya u'genius wake.

Rest In Paradise Genius Zilla.

Ndimi Luqman MALOTO