Ugonjwa wa Vitiligo: Chanzo, Dalili na Tiba - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Feb 2019

Ugonjwa wa Vitiligo: Chanzo, Dalili na Tiba


Ni moja ya magonjwa ya kudumu ya ngozi unaosababishwa na kinga za mwili kujishambulia (autoimmune reaction) na kuathiri seli za melanocytes (melanini), zinazotengeza rangi ya ngozi na kusababisha mabaka meupe katika baadhi ya maeneo ya mwili
-
Huweza kutokea sehemu yoyote ya mwili, hausababishwi na bakteria wala vijidudu na huweza kuathiri familia au ukoo fulani. Wagonjwa wengi huathirika zaidi katika maeneo yanayopigwa na jua kama vile usoni, mikononi na shingoni
-
Tofauti na ilivyo kwa maradhi mengine, mgonjwa wa vitiligo hapati dalili zozote mfano maumivu, kuwashwa au homa bali huanza kuona mabaka meupe au madoa yakijitokeza katika ngozi yake
-
Vitiligo hauchagui umri wala jinsia na mara nyingi huwapata vijana ingawa uwezekano mkubwa ni kuwapata watu wenye umri kati ya miaka 20 mpaka 40. Kwa mtu mwenye chembechembe za ugonjwa huu, mpaka anapofikisha miaka 40 tayari dalili zake zitakuwa zimeshajitokeza
-
Mgonjwa ana uwezekano mkubwa wa kupata saratani ya ngozi pindi akipigwa na mwanga wa jua hasa kwenye sehemu zilizoathirika jambo ambalo hutakiwa kuwa makini nalo wakati wote
-
Kwa sasa, ugonjwa huu hauna tiba ya uhakika bali zipo dawa za kupaka ili kupunguza kasi ya kusambaa kwake. Matumizi ya vipodozi husaidia kuficha maeneo yaliyoathirika na kuzuia ngozi isidhurike