Isabela Achekelea Adhabu Aliyopewa Mwanamuziki Shilole na Basata - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Aug 2015

Isabela Achekelea Adhabu Aliyopewa Mwanamuziki Shilole na Basata

BAADA ya msanii na muigizaji Zuwena Mohamed ‘Shilole’ kufungiwa na Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kwa kitendo chake cha kucheza nusu utupu jukwaani, msanii mwenzake Isabela Mpanda amechekelea adhabu hiyo na kusema liwe fundisho kwa wengine.

Akipiga stori na gazeti hili, Isabela alisema pamoja na kumhurumia juu ya maisha atakayoishi bila kufanya kazi kwa mwaka mzima wa kutumikia adhabu yake, lakini hatua hiyo ni nzuri kwani wapo wengi wenye tabia ya kucheza na kuacha matiti nje.

Mimi huwa sivai nguo inayoniacha matiti wazi, kwa nini wasanii hawafanyii majaribio kwanza ya nguo kabla hawajavaa na kutoka? Ninamhurumia na nampa pole maana sijui atawaleaje watoto wake watatu, maana anautegemea muziki katika kuendesha familia yake,” alisema Isabela.