Kigogo Ikulu Aokoa Jahazi...Azuia Nyumba ya Mwanamuziki Lady Jide Dee Kuuzwa - MULO ENTERTAINER

Latest

5 Aug 2015

Kigogo Ikulu Aokoa Jahazi...Azuia Nyumba ya Mwanamuziki Lady Jide Dee Kuuzwa

KISMATI! Ile nyumba ya nyota wa muziki wa kizazi kipya nchini, Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ iliyopo Mivumoni, Kinondoni jijini Dar es Salaam, iliyowekwa mnadani zaidi ya mwezi mmoja uliopita, imezuiwa kupigwa bei na kigogo mmoja wa ikulu, Risasi Mchanganyiko lina full data.

Habari kutoka chanzo cha kuaminika zinasema kigogo huyo ambaye kutokana na hadhi yake hawezi kutajwa jina, mara baada ya kupata taarifa za mnada huo, alimuagiza mmoja wa wasaidizi wake kutafuta namba ya msanii huyo, ambaye wakati huo alikuwa China kwa shughuli zake binafsi.
Mzee alisikia kama nyumba ya Jide inauzwa, akawa anatafuta namba yake ili azungumze naye ajue tatizo nini, anaonekana anataka kumsaidia ili jambo hilo limalizike, bado sijajua kama atamsaidia hela au kumuombea muda zaidi wa kulipa deni hilo,” kilisema chanzo chetu.

Baada ya kupata ‘ubuyu’ huo, gazeti hili lilitaka kujiridhisha na ukweli wa habari hizo na lilipowasiliana na mmoja wa maofisa wa kampuni ya udalali ya Mem Auctioneers And General Brokers Ltd, waliotangaza mnada huo, alikiri kusitishwa kwa zoezi hilo.

Ni kweli zoezi limesitishwa, tulitaarifiwa na wateja wetu, taasisi ya fedha ya EFC TANZANIA LTD kwa kuambiwa kuwa wameshamalizana na msanii huyo, hatujui kama alilipa au kulikuwa na makubaliano mengine, lakini hilo suala la mkubwa kuzuia sisi hatulifahamu,” alisema ofisa huyo, aliyejitambulisha kwa jina la Mushi Dalali.