Yanga Inaweza Kuadhibiwa na CAF - Malinzi - MULO ENTERTAINER

Latest

1 Jul 2016

Yanga Inaweza Kuadhibiwa na CAF - Malinzi

Rais wa TFF amesema bado wanasubiri taarifa kutoka CAF juu ya vurugu zilizotokea nje ya uwanja muda mchache kabla ya mchezo huo kufanyika huku akisema Yanga wasubiri kudra za Mwenyezi Mungu ili kuepuka adhabu kutoka shirikisho hilo la soka Afrika.

Hata hivyo Malinzi amesema Yanga bado ina nafasi ya kufuzu nusu fainali ya michuano hiyo kutokana na namna kundi lao lilivyo hadi sasa hivyo wao kama shirikisho wanawatakia kila la kheri katika maandalizi yao.