Prof. Mwandosya: Kuuliza si Ujinga, kamati za Bunge Kutowasilisha Ripoti Bungeni Kwanza, Je Kanuni zimebadilika? - MULO ENTERTAINER

Latest

10 Sept 2017

Prof. Mwandosya: Kuuliza si Ujinga, kamati za Bunge Kutowasilisha Ripoti Bungeni Kwanza, Je Kanuni zimebadilika?

Mwanasiasa mkongwe na waziri mwandamizi wa zamani, Prof Mark Mwandosya ameandika katika "tweet" akihoji kuwa,huu utaratibu wa kamati ya Bunge kuundwa na Spika kuchunguza jambo fulani,na baadae badala ya kuliwasilisha bungeni na wabunge kupata muda wa kujadili,safari hii kamati zimewasilisha taarifa zao nje ya bunge lakini katika viwanja vya bunge,na baadae taarifa hiyo kukabidhiwa kwa Rais.

Prof Mwandosya anahoji anasema "Je Kanuni za Bunge zimabadilika?"...Maana ilivyozoeleka na kwa mujibu wa kanuni, kamati kama hizi huwasilisha taarifa zao ndani ya bunge, bunge hujadili na baadae kutoa maazimio ambayo Serikali hupaswa kuyafuata na kuyatekeleza.

Hivi ndivyo ilivyofanya kamati ya Mwakyembe juu ya suala la Richmond, Kamati ile ya Operesheni Tokomeza na hata kamati hizi mbili za kuchunguza Tanzanite na Almasi zilipaswa kufanya hivyo kwa mujibu wa kanuni za kudumu za Bunge.