Amuua Baba na Mama yake pamoja na Mkewe na yeye kujiua - MULO ENTERTAINER

Latest

29 May 2018

Amuua Baba na Mama yake pamoja na Mkewe na yeye kujiua

Matukio ya mauaji ya kutumia risasi yanaendelea kujitokeza nchini Marekani ambapo kumezuka vurugu na ufyatulianaji wa risasi katia nyumbani moja na kuacha watu wanne wamefariki katika jimbo la Tennessee.

Sheriff Mike Fitzhugh amesema mwanamume mwenye umri wa miaka 38 alimpiga risasi mke wake, baba yake na mama yake wa kambo, kabla ya kujiua.

Fitzhugh amesema mtu huyo alikuwa amepelekwa hospitali baada ya kutoa mawazo ya kujiua, na silaha zote zilikuwa zimeondolewa katika makazi yao. Lakini haijulikani yaliyotokea mwishoni mwa wiki.

Kesi iko chini ya uchunguzi zaidi.