UONGOZI wa Azam FC umeweka bayana kuwa, kocha wa timu ya Singida United, Mholanzi, Hans van Der Pluijm, ndiye aliyeandika barua ya maombi ya kuifundisha timu yao tangu akiwa Yanga.
Pluijm ambaye ameanza kuinoa Singida United msimu huu, taarifa za uhakika zinasema kuwa Mholanzi huyo ameshasaini mkataba wa miaka miwili na matajiri hao wa Chamazi.
Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Azam FC, Philipo Alando, alisema kuwa kocha huyo ndiye aliyeandika barua kuwa anataka kuifundisha klabu hiyo tangu kipindi anaifundisha Yanga.
“Pluijm yeye ndiye aliyeandika barua kuwa anatamani kuja kutufundisha na mara ya kwanza aliandika akiwa anaifundisha timu ya Yanga kwa vile amemaliza mkataba na Singida ndiyo maana watu wanamhusisha kuja kwetu ila sisi huwa hatufichi kitu kama mlivyoona kwa Ngoma (Donald), sisi huwa tunaweka vitu hadharani,” alisema Alando.
29 May 2018
New