Baada ya Kipigo Kocha wa Yanga Aisifu Simba - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Feb 2019

Baada ya Kipigo Kocha wa Yanga Aisifu Simba

Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amekisifu kikosi cha klabu ya Simba na kusema Wachezaji wa Yanga walikosa ubunifu ndio maana wamepoteza mchezo wa jana
-
Zahera amesema ushindi wa jana wa Simba dhidi ya timu yake unakuja wakati ambapo klabu hiyo ya Msimbazi ingeshinda tu maana kwa sasa inacheza vizuri
-
Amesema timu yake ina Wachezaji wazuri lakini wanakosa ubunifu ule wa utafuta suluhisho la namna ya kucheza na kufunga magoli tofauti na ilivyo kwa Wachezaji wa Simba wenye uwezo huo
-
Hata hivyo amesisitiza kuwa bado Simba inafungika kirahisi sana na msimu ujao timu yake ya Yanga itamfunga Simba
-
Katika mchezo wa jana Klabu ya Simba iliibuka na ushindi wa goli 1 - 0,  goli lililofungwa dakika ya 71 na Meddie Kagere