Jumatano ya January 14, kwenye XXL ya Clouds FM Soudy Brown amepiga story na muigizaji Aunty Ezekiel kuhusiana taarifa kwamba ni mjamzito na ameonekana akinywa pombe,
Soudy alimuuliza kama anafahamu athari za kunywa pombe huku akiwa na ujauzito, Aunty akasema hazijui na yeye sio mjamzito.
Soudy alimtafuta pia Dk Makongoro kutoka Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye alielezea kuhusu matatizo ambayo mwanamke anaweza kuyapata iwapo ni mjamzito na anatumia pombe kali,
Daktari huyo amesema kuwa mama mjamzito anatengeneza mazingiza ya pombe kusafiri kutoka kwake kwenda kwa mtoto na kujitunza kwenye sehemu za ubongo kitendo kinachosababisha mtoto kuzaliwa akiwa na matatizo kama mtindio wa Ubongo, Kuzubaa au matatizo ya macho.
----------------------
'You've gotta dance like there's nobody watching,
Love like you'll never be hurt,
Sing like there's nobody listening,
And live like it's heaven on earth.'