Kamwe Sitafuti Kiki Nirudi Kwenye Chat ya Music....Nina Biashara Zangu Zinazoniingizia Pesa Nyingi - Dudu Baya - MULO ENTERTAINER

Latest

17 Mar 2016

Kamwe Sitafuti Kiki Nirudi Kwenye Chat ya Music....Nina Biashara Zangu Zinazoniingizia Pesa Nyingi - Dudu Baya

Msanii Dudu baya amesema kwamba katika maisha yake hawezi kutafuta kiki ya kurudia kwenye game, kwani ana biashara yake inayomuingizia pesa nyingi zaidi.

Dudu Baya ameyasema hayo alipokuwa akiongea kwenye stori 3 za Planet Bongo inayorushwa na East Africa Radio, na kusema kuwa ana biashara na kampuni, na hivi karibuni anafikiria kuleta wasanii wakubwa kutoka nje.


"Nikifungua bar ni mambas, kwa sasa nina kampuni ya Mambas Entertainment, nimeanza kazi muda mrefu naweza kuongea na msanii tukaenda Musoma tunapiga show, na may dream nitakuwa nawaleta hata wasanii kutoka nje, lakini sasa hivi toka 2013 niko kanda ya ziwa, na ndio maana hata show zangu sitegemei nipigiwe show na promota", alisema Dudu Baya.

Pamoja na hayo Dudu Baya amesema shughuli za ujenzi na biashara ya mbao, ndio inayomfanya asisikike kwenye muziki kwa sasa.


"Mi nimesomea archteck uchoraji wa majengo na ujenzi, natoa mbao Kasulu, ukiona sisikiki kwenye muziki ujue hiyo ndio business im doing", alisema Dudu Baya.