Rais Magufuli kapiga simu kwenye kipindi cha TV ya Tanzania kwa mara ya kwanza tangu awe Rais (sauti) - MULO ENTERTAINER

Latest

18 Mar 2016

Rais Magufuli kapiga simu kwenye kipindi cha TV ya Tanzania kwa mara ya kwanza tangu awe Rais (sauti)

Kwenye zile kubwa ambazo zimenifikia leo March 17 ni pamoja na hii ya Rais wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kuvutiwa na kipindi cha Clouds 360 cha Clouds Tvmpaka akaamua kuwapigia simu moja kwa moja studio na kuwapongeza.
Kingine alichokisema Rais Magufuli ni  kuwa yeye ni shabiki namba moja wa kipindi hicho na anafurahishwa na kazi nzuri inayofanywa na Clouds Media Group kama zoezi zima la MalkiaWaNguvu na mengine mengi.
Rais Magufuli ambaye wakati anapiga simu studio alikua na Mke wake Mama Janeth Magufuli,amewapongeza Watangazaji wa kipindi hicho Hudson Kamoga,Babie Kabae naSam Sasali kwa jinsi wanavyokifanya vizuri kipindi hicho hasa kwenye uchambuaji wa Magazeti wa kipindi hicho.
Nimeinasa pia sauti ya Rais Magufuli akiongea live kwenye kipindi cha Clouds 360.