Dimpoz Afunguka Kuhusu Mubenga - MULO ENTERTAINER

Latest

21 Nov 2016

Dimpoz Afunguka Kuhusu Mubenga

Msanii Ommy Dimpoz amekanusha tetesi za kuwa na ugomvi na aliyekuwa ‘business partiner’ ambaye pia alikuwa meneja wake maarufu kwa jina la Mubenga, baada ya kila mmoja kuchukua hamsini zake na kufanya yake.

Akizungumza kwenye FNL ya East Africa Television Ommy Dimpoz amesema Mubenga ameamua kufanya biashara zake mwenyewe bila kushirikiana naye, kitu ambacho ni jambo zuri kwake na kwa maendeleo pia, lakini hawana tofauti na hata akihitaji msaada wake, yupo tayari kumsaidia.

“Mubenga ameenda kuanzisha kitu chake, hiyo ni pongezi na hayo ni maendeleo, mnataka kila siku awe chini ya Ommy! yeye ameenda kuazisha kitu chake, kampuni yake, ana wasanii wake anawasimamia, anajua kwamba afanye vipi anahitaji ku’move on’, kwa hiyo ilikuwa ni movement yake yeye kwamba ameamua kufanya kazi zake mwenyewe which is good, na mimi hata leo akisema Ommy nataka suport hii kwa wasanii wangu i’m ready”, alisema Ommy Dimpoz.

Ommy Dimpoz amesema hata tetesi za kuchukua hela za Mubenga na gari hazina ukweli wowote, ni maneno tu ya uzushi ya mashabiki, na bado anamchukulia kama ndugu yake.