Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli amesema alitamani kuhudhuria tamasha la muziki la Fiesta ambalo litafanyika Jumamosi hii katika viwanja vya Leaders Club.
Akiongea na waandishi wa habari Ijumaa hii Ikulu jijini Dar es salaam, Magufuli alisema alitamani kuhudhuria tamasha hilo ili apige tumba lakini majukumu ya kazi yamembana.
“Natamani kwenda Fiesta siku ya kesho sema hii kazi inanibana kwa kuwa itakuwa live nitaifuatilia kupitia kwenye runinga,” alisema Magufuli.
Pia Rais huyo ambaye kesho November 5 anatimiza mwaka mmoja toka aingie madakani, alimmwagia sifa msanii wa muziki wa asili Mrisho Mpoto kwa kufanya muziki wenye maadili na kuelimisha.
4 Nov 2016
New
mulo
MAGUFULI