Mwanamitindo Mtanzania Flaviana matata ambaye Novemba 2014 alichumbiwa, amesema kuwa hata atakapoolewa, ndoa haitabadilisha au kuathiri chochote katika kazi zake.
“Kila kitu kitaendelea kama kilivyo sasa mpaka pale nitakapoona sasa imetosha nifanye mambo mengine, lakini haitabadilisha chochote, itabadilisha status tu ndo inakuwa mrs flani basi.” Alisema kupitia XXL ya Clouds Fm.
Mwanamitindo huyo wa kimataifa ambaye hufanyia shughuli zake Marekani, hajataka kumuweka wazi mchumba wake lakini amesema ni Mtanzania anayeishi Marekani.
Baada ya kuulizwa kwanini amechagua kuolewa na Mtanzania mwenzake, alijibu hiki: