LICHA ya Beautiful Onyinye, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ kuwahi kufikishwa kortini na Mbongo Fleva, Raheem Rummy Nanji ‘Bob Junior, wamebambwa ‘live’ wakioneshana mahaba niue, Amani lina tukio zima.
Ishu hiyo iliyopigwa chabo na paparazi wetu hivi karibuni lilijiri ndani ya Ukumbi wa Club 71 uliyopo Tegeta jijini Dar es Salaam ambapo Wema siku hiyo alimtambulisha msanii wake mpya anayesimamiwa na kampuni yake ya Endless Fame anayeitwa Ally Luna.
Katika tukio hilo, Wema ndiye aliyeanza kufika ukumbini humo akifuatana na timu yake, akiwemo Petit Man (kama kawa).
Muda mfupi baadaye, Bob Junior naye alifika ambapo alipokutana na Wema walianza kupeana mahaba huku wakigandana kwa zaidi ya dakika kumi.
Katika tukio hilo, kilichowashangaza mashuhuda zaidi ni kitendo cha Wema kukaa mapajani kwa Mbongo Fleva huyo bila kujalia macho ya watu.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo walikwenda mbali zaidi na kuanza kuhisi tabia hiyo ya Wema na Bob Junior ni salamu kwa aliyekuwa mwandani wake na kumwagana Nasibu Abdul ‘Diamond’ na ‘bebi’ wake wa sasa, Zarinah Hassan ‘Zari’.
“Hapa naona kama sielewielewi maana ni mara ya kwanza kumwona Wema na Bob Junior wakigandana kiasi hiki tangu walipopelekana mahakamani kipindi kile na ukizingatia Sharobaro (Bob Junior) alikuwa hasimu wa Diamond aliyekuwa mpenzi wa Wema kipindi hicho,” alisema mmoja wa mastaa wakubwa (jina linahifadhiwa). Akaongeza:
“Nakuhakikishia hizi ni salamu kwa Diamond na yule Zari wake. Hapa Wema anajua kabisa salamu zitawafikia.”
Baadhi ya mastaa hao walionekana kulaani tukio hilo na kujaribu kumtahadharisha Wema juu ya ukaribu huo kwani kama Diamond atagundua atajua ni ishu za kulipizana visasi.
“Kwa vyovyote Diamond akigundua jambo hili litamfanya ukaribu wake na Wema kuzidi kuwa mgumu na kuurejesha ni ndoto kama wana mpango wa kurudiana.”
Paparazi wetu alipojaribu kuwadodosa wawili hao juu ya uhusiano wao, kila mmoja aliishia kucheka tu bila kutoa majibu ya kueleweka.
17 Jan 2015
New